Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI

Wananchi wa Iran waandamana kuashiria miaka 34 ya shambulio kwenye ubalozi wa Marekani

Mamia ya wananchi wa Iran wameandamana kuashiria kumbukumbu ya miaka 34 tangu kutokea kwa tukio la kutekwa kwa ubalozi wa Marekani, na kusababisha kutatizika kwa uhusiano baina ya nchi hizo mbili. 

Baadhi ya waandamanaji mjini Tehran wakichoma moto bendera ya Marekani
Baadhi ya waandamanaji mjini Tehran wakichoma moto bendera ya Marekani thegatewaypundit.com
Matangazo ya kibiashara

Licha ya mahusiano yanayoonekana kuboreshwa na utawala mpya nchini Iran na Marekani, serikali ya Iran inaadhimisha kumbukumbu hiyo ya miaka 34 huku ikiendelea na kauli mbiu yake ya kifo cha Marekani.

Katika tukio hilo kundi la wanafunzi wa Kiislam walivamia ubalozi wa Marekani na kuwateka wanadiplomasia 52 kwa muda wa siku 44,tukio ambalo lilisababisha kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.

Wito wa kujitokeza kwa wingi katika maandamano hayo umetolewa kupitia televisheni licha ya kuvunjika kwa uadui hivi karibuni kati ya mataifa hayo kufuatia mawasiliano ya simu baina ya marais wa nchi hizo mbili.

Maandamano makubwa yamefanyika mbele ya jengo la zamani la ubalozi wa Marekani mjini Tehran, huku waandamanaji wakipunga hewani mabango yanayopiipinga Marekani huku wakiimba kauli mbiu isemayo kifo cha Marekani na kifo cha Israel kisha kuchoma bendera za mataifa hayo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.