Pata taarifa kuu
SYRIA

Shirika la kimataifa la kupambana na silaha za Kemikali laharibu vifaa vya Syria

Shirika la Kimataifa linaloshughulika na silaha za Kemikali duniani OPCW linasema kuwa limeharibu vifaa vyote vinavyotumiwa kutengeneza silaha za kemikali nchini  Syria.

Matangazo ya kibiashara

OCPW limetoa kauli  hiyo siku moja kabla ya siku ya mwisho ya tarehe 1 mwezi Novemba  iliyokuwa imepangwa na shirika hilo kuharibu viwanda vyote vya kutengeneza silaha hizo hatari.

Mpango wa kuharibu silaha za kemikali za serikali ya Syria ulikubaliwa kati ya serikali ya Marekani na Urusi kama njia mojawapo ya kumaliza mzozo huo na kuzuia uwezekano wa Damascus kuendelea kutumia silaha hizo kuwashambulia raia wake.

Serikali ya Israel sasa ina hadi katikati ya mwaka ujao kuteketeza silaha zake zote za kemikali ambazo ni zaidi ya Tani 1,000.

Mwezi Agosti mwaka huu, serikali ya rais Assad ilitumia kutumia silaha hizo kuwashambulia wapinzani karibu na mji wa Damascus shambulizi ambalo lilisababisha Marekani kutishia kuishambulia Syria kijeshi.

Katika hatua nyingine, rais  Bashar Al Assad amesema kuwa yuko tayari kwa mazungumzo ya amani na wapinzani iwapo tu mataifa kutoka nje hayataingilia katika mchakato huo.

Assad alimwambia Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na nchi za kiarabu Lakhdar Brahimi jijini Damascus kuwa ni wananchi wa Syria ndio waliona na uwezo wa kuamua mustakabli wa taifa lao.

Aidha, Damascus imesisitiza kuwa haitashiriki katika mazungumzo yoyote na upinzani ambao bado unamiliki silaha kauli ambayo imedhoofisha matumaini ya kufanikisha mazungumzo hayo.

Upinzani kwa upande wao  nao unasema kuwa hautakubali kuzungumza na uongozi wa rais Assad na kusisitiza kuwa mazungumzo kama hayo yanaweza tu kufanyika ikiwa rais Assad atajiuzulu kwanza.

Balozi wa Iran nchini Syria Mohammad Riza Shebani, alinukuliwa akisema kuwa nchi yake iko tayari kushiriki katika mazungumzo hayo yaliyopangwa kufanyika tarehe 23 mwezi Novemba.

Kabla ya kuzuru Syria, Brahimi amekuwa nchini Iraq, Misri, Kuwait, Oman , Qatar na Iran alikokutana na rais Hassan Rouhani katika haraka za kuomba uungwaji wa kufanyika kwa mazungumzo hayo.

Ripoti kutoka Damascus zinaeleza kuwa wakati Brahimi akiwa katika ziara hiyo mapigano makali kati ya jeshi la serikali na waasi yanaendelea karibu na jiji hilo kuu.
Wiki iliyopita, Brahimi alikutana na Jeshi huru la Syria nchini Uturuki na viongozi wengine wa kijeshi.

Machafuko nchini Syria yamekuwa yakiendelea kwa mwaka wa pili sasa na zaidi ya watu 100,000 wamepoteza maisha na zaidi ya Milioni moja kukimbia makwao.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.