Pata taarifa kuu
URUSI-MAREKANI

Edward Snowden atembelewa na babake nchini Urusi

Baba wa aliyekuwa Jasusi wa Marekani Edward Snowden anayesakwa na serikali ya Marekani amewasili nchini Urusi kumtembelea mwanaye.

Matangazo ya kibiashara

Lon Snowden amewaambia waandishi wa Habari jijini Moscow kuwa anafuraha ya kuwa na kumwona mwanaye ambaye amesema yuko katika hali nzuri na salama nchini humo.

Edward Snowden alipewa hifadhi ya kisiasa nchini Urusi mwezi Agosti baada ya kukwama katika uwanja wa ndege kwa wiki kadhaa baada ya serikali ya Marekani kuanza kumsaka.

Baba wa Snowden amesema kuwa hawezi kufahamu ikiwa mwanaye atarudi nyumbani au la kwa kile alichosema kuwa uamuzi ni wake kwa sababu yeye ni mtu mzima sasa.

Raia huyo wa Marekani anatakiwa na Serikali ya rais Barack Obama kwa kuvujisha siri muhimu za Shirika la Ujasusi kuhusu kuchunguzwa kwa mawasiliano ya simu yanayofanywa na jeshi la Marekani.

Snowden alivujisha siri hizo zilizochapishwa katika vyombo vya habari nchini Marekani kama gazeti la The Guardian na Washington Post na kuzua mjadala mkubwa kuhusu uhuru na usalama wa mawasiliano ndani na nje ya Marekani.

Jasusi huyo wa zamani anatuhumiwa na serikali ya Marekani kwa wizi wa habari za siri za serikali na kutoa habari muhimu  kinyume cha sheria za kijeshi nchini humo katika makosa ambayo ikiwa atapatikana na kosa afungwa jela miaka 10 kwa kila kosa.

Hatua ya Snowden kupewa hifadhi ya kisiasa nchini Urusi imetikisa uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Marekani na Urusi katika siku za hivi karibuni huku serikali ya rais Obama ikiituhumu Moscow kwa kumhifadhi mhalifu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.