Pata taarifa kuu
KENYA

Kiongozi wa Kidini anayetajwa kuhubiri itikadi za Kundi la Al Shabab auawa nchini Kenya na watu wenye silaha

Hofu ya usalama imeendelea kutanda Mjini Mombasa nchini Kenya kufuatia watu wenye silaha kumuua Kiongozi maarufu wa Dini ya Kiislam Sheikh Ibrahim Ismail pamoja na wafuasi wake wanne walipokuwa wanarejea nyumbani wakitoka Msikitini. Sheikh Ismail ambaye alikuwa mrithi wa Abdoud Rogo Mohammed amekuwa akitajwa kuwa msambazaji wa itikadi za Kundi la Wanamgambo la Al Shabab la nchini Somalia linalotajwa kutekeleza mashambulizi ya kujitoa mhanga nchini Kenya.

Gari alilokuwa anatumia Kiongozi wa Kidini huko Mombasa Sheikh Ibrahim Ismail likiwa limezingirwa na watu baada ya kupigwa risasi
Gari alilokuwa anatumia Kiongozi wa Kidini huko Mombasa Sheikh Ibrahim Ismail likiwa limezingirwa na watu baada ya kupigwa risasi
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa kidini ambaye alikuwa anaongoza Msikiti wa Musa unaotajwa kuwa na itikadi kali amekuwa akitoa mahubiri yanayotajwa kuchochea wananchi wengi nchini Kenya kujiunga na Kundi la Al Shabab.

Sheikh Ismail ameuawa kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Sheikh Rogo aliyeuawa akituhumiwa kuwa Msemaji wa Kundi la Al Shabab nchini Kenya na aliuawa mwezi Agosti mwaka 2012.

Jeshi la Polisi limethibitsha Sheikh Ismail akiwa na wenzake wanne walishambuliwa na watu wenye silaha wakiwa kwenye gari lao na kupoteza maisha kisha watu hao wakatokokea kusikojulikana.

Polisi wameendelea kusema mwili wa Sheikh Ismail ulikutwa umejawa na damu kutokana na mashambulizi ya risasi yaliyofanywa na watu hao waliokua wamejihami vilivyo kwa silaha nzito.

Wafuasi wa Sheikh Ismail wamejitokeza na kulituhumu Jeshi la Kenya kuhusika kwenye mauaji ya Kiongozi wao tuhuma zilizokanusha vikali na Jeshi la Polisi linaodai hajahusika kwa namna yoyote.

Hofu imeanza kuzagaa huenda kukafanyika maandamano makubwa kwenye Mji wa Mombasa mchana wa leo kuonesha hasira za wafausi wa Sheikh Ismail kufuatia kifo cha Kiongozi wao wa Kidini.

Sheikh Ismail amekuwa mstari wa mbele kuhubiri siasa za Kundi la Wanamgambo la Al Shabab huko Mombasa na kuwashawsihi vijana wengi kuwa tayari kujiunga na kundi hilo linalotajwa kuwa kitisho cha usalama nchini Kenya.

Mtangulizi wake Sheikh Rogo wakati wa uhai wake alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa kwenye orodha ya watu waliowekewa vikwazo na Marekani pamoja na Umoja wa Mataifa UN.

Kundi la Wanamgambo la Al Shabab limeendelea kuwa hatari baada ya kjutekeleza shambulizi lililochangia vifo vya watu sitini na saba baada ya kuliteka Jumba la Biashara la Westgate.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.