Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI-URUSI-UN

Ban asema mazungumzo kuhusu amani nchini Syria huenda yakapangwa kufanyika mwezi Novemba

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon jana Ijumaa amearifu kuwa mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakitafutwa kwa muda mrefu kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini Syria huenda yakapangwa kufanyika mwezi Novemba. 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon REUTERS/Andrew Burton/Pool
Matangazo ya kibiashara

Ban ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kupitisha azimio la kihistoria dhidi ya silaha za kemikali nchini Syria.

Ban ameongeza kuwa mjumbe wa amani wa umoja wa mataifa na jumuiya ya nchi za kiarabu nchini Syria Lakhdar Brahimi atafanya kazi ya maandalizi itakayohitajika majumakadhaa kabla ya kuwaleta pamoja upinzani na utawala wa Rais Bashar al-Assad.

Wakati hayo yakijiri wataalam wa Umoja wa Mataifa nchini Syria wanachunguza mashambulizi saba yanayodaiwa kutumia silaha za kemikali na wanatarajia kumaliza kazi yao nchini humo siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa jana Ijumaa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.