Pata taarifa kuu
KENYA-ICC

Rais Uhuru Kenyatta awahakikishia wakenya serikali imara licha ya kesi inayo mkabili yeye na naibu wake huko Hague

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewahakikishia wakenya kuwa uongozi wa serikali yake utaendelea kuwahudumia wakenya, licha ya kesi zinazomkabili yeye na naibu rais William Ruto katika mahakama ya ICC jijini Hague huko Uholanzi, ambapo pia mwanahabari Joshua Arap Sang anakabiliwa na baadhi ya mashtaka kuhusiana na ghasia zilizoibuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. 

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. REUTERS/How Hwee Young/Pool
Matangazo ya kibiashara

Rai Kenyatta amewataka wakenya kutotiwa hofu na maneno ya watu wanaotaka kutumia nafasi hiyo kueneza uvumi kuwa Kenya haitakuwa na uongozi ikiwa rais Kenyatta na naibu wake watakapo elekea huko Hague badala yake amewaambia kuwa wao hawana hatia na anaamini watashinda na ushindi huo utakuwa wa wakenya.

Wakati hayo yakijiri jijini Nairobi huko Mombasa mdahalo kuhusu hatua ya wabunge wa Kenya kupitisha hoja ya kutaka taifa hilo kujitoa katika mkataba wa Roma uliobuni mahakama ya kimataifa ya ICC, bado unaendelea kupingwa na wananchi wakiwemo viongozi mbali wa kisiasa nchini humo.

Makamu wa zamani wa rais Kalonzo Musyoka amesema kuwa suala la kujiondoa katika mkataba wa Roma unaitangaza vibaya nchi hiyo kimataifa.

Rais Kenyata na Naibu wake William Ruto wamepangiwa kuhudhuria baadhi ya vikao vya kesi zao kwa pamoja baadaye mwezi huu ambapo naibu Ruto anatarajia kuondoka nchini Kenya Jumatatu juma lijalo kuelekea Hague Uholanzi ambapo rais Kenyatta atafuata baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.