Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA

Mawaziri wa kigeni wa Umoja wa Ulaya watoa wito kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya rais wa Syria

Marekani na Ufaransa zimedai kuwa kumekuwa na ongezeko la uungwaji mkono kimataifa kuhusu kuingilia kijeshi nchini Syria kama hatua ya kuiadhibu nchi hiyo kwa madai ya kutumia silaha za kemikali. 

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry akiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry akiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya themalaysianinsider.com
Matangazo ya kibiashara

Washington na Paris kwa pamoja zimesema kuwa nchi nyingine zaidi zimekuwa nyuma ya uhitaji wa hatua za kuingilia kijeshi kuchukuliwa baada ya mataifa ya Umoja wa Ulaya kulaani matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria waliyoyaita ya kijinga.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema idadi ya nchi ambazo ziko tayari kuchukua hatua za kijeshi sasa imeongezeka mara mbili,baada ya kufanya mazungumzo na mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya huko Lithuania.

Kufuatia mkutano na mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya, mawaziri hao wametoa wito kwa hatua kuchukuliwa dhidi ya rais wa serikali ya Syria Bashar al Assad.

Marekani inaituhumu serikali ya Assad kwa kuwashambulia watu zaidi ya 1400 kwa silaha za kemikali katika shambulio la Agosti 21 nje ya mji wa Damascus.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.