Pata taarifa kuu
IRAQ

Watu zaidi ya 50 wauawa kwa kushambuliwa na mabomu nchini Iraq

Mashambulizi kadhaa ya mabomu yametokea nchini Iraq na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 50 na mamia kujeruhiwa.

Matangazo ya kibiashara

Polisi nchini humo wanasema kuwa mashambulizi hayo yalilenga ngome za Waislamu wa Kishia wakati walipokuwa katika harakati za kwenda kazini huku wengine wakijishughulisha na mambo mengine.

Kiwango cha machafuko kimeongezeka nchini Iraq katika siku za hivi karibuni kutokana na uhasama unaoendelea kukithiri kati ya Waislamu wa Kishia na wale wa Wasunni.

Polisi wanasema kuwa zaidi ya milipuko 10 ya bomu ilitokea siku ya Jumatano katika maeneo mbalimbali ikiwemo Wilaya ya Jisr Diyala mjini Baghdad na mji wa Sadr.

Hadi sasa hakuna kundi lililojitokeza kudai kutekeleza mashambulizi hayo lakini polisi wanashuku kuwa yalitekelezwa na wapiganaji wa Kisunni.

Waislamu wa Kisunni wanasema kuwa wanatengwa na serikali ya Waziri Mkuu Nouri Maliki ambaye anaongoza serikali ya Kishia tuhma ambazo serikali inapinga na kusema kuwa wapiganaji hao wanatumiwa na makundi ya kigaidi.

Tangu kuanza kwa mwaka huu, zaidi ya watu 4,000 wameuawa na zaidi ya 10,000 kujeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo ya mabomu.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa mwezi Julai ullikuwa mbaya sana kwa raia wa Iraq baada ya watu 1,057 kupoteza maisha yao wengi wao wakiwa mjini Baghdad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.