Pata taarifa kuu
DRCongo-Rwanda

Serikali ya Rwanda na tuhuma kwa jeshi la FARDC kurusha makombora katika ardhi yake, Monusco yatowa tahadhari kwa waasi wa M23 kwa mashambulizi dhidi ya raia

Serikali ya Rwanda imelituhumu jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo la FRDC kurusha roketi zilizolenga hadi maeneo ya mpakani na kuongeza kuwa tukio hilo ni la uchokozi. Msemaji wa jeshi la Rwanda, Joseph Nzabamwita amethibitisha kurushwa kwa roketi hiyo toka upande wa majirani zao nchini ya DRC na kwamba makombora hayo yalirushwa kwa makosudi ndani ya ardhi ya Rwanda na wanajeshi wa Serikali ya DRC.

Kiongozi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRCongo, Martin Kobler
Kiongozi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRCongo, Martin Kobler
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo ya kurushwa kwa Makombora katika ardhi ya Rwanda inakuja ikiwa ni siku moja tu imepita toka kushuhudiwa kuanza kwa mapigano mapya kwenye mji wa Goma kati ya wanajeshi wa Serikali na wale wapiganaji waasi wa kundi la M23 ambapo raia kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa.

Watu watatu wanaripotiwa kujeruhiwa vibaya jana katika kata ya ofisi ilio kaskazini mwa jiji la Goma na Makombora yaliorushwa katika mji huo. Kiongozi mmoja wa jiji hilo ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema watu hao wapo katika hjali mbaya. Hata hivyo amejizuia kutowa taarifa zaidi kuhusu makombora hayo.

Mashambulizi hayo yamezua hisia kubwa kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini DRCongo vinavyo dai kulengwa katika mashambulizi hayo, hali iliyo mfanya mkuu wa Monusco nchini DRCongo Martin Kobler kutowa taarifa ambamo amelitahadharisha kundi la waasi wa M23 na kusema kwamba hawato vumulia mashambulizi yoyote dhidi ya raia.

Martin Kobler amesema juwa ametowa amri kwa vikosi vya Monusco kujibu mashambulzi yoyote yatayo lenga raia na kuchukuwa hatuwa za tahadhari kwa ajili ya kuwalinda raia na kuzuia waasi wa M23 kusonga mbele.

Mapambano kati ya vikosi vya serikali ya DRCongo FARDC na vile vya waasi wa M23 yanaripotiwa tangu siku ya jumatano jioni karibu na vijiji vya Mutaho na Kibati kwenye umbali wa zaidi ya kilometa hamsini na jiji la Goma. Kila upande unamtuhumu mwingine kuanzisha mashambulizi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.