Pata taarifa kuu
MAREKANI

Rais Obama amtaka rais Putin kusahau yaliyopita licha ya mvutano wao kuhusu Snowden

Rais wa Marekani Barack Obama ameijibu Urusi kuhusu hatua yake ya utoaji wa hifadhi kwa mfanyakazi wake wa zamani wa shirika la kijasusi anayedaiwa kuvujisha siri za shirika hilo Edward Snowden sambamba na sheria yake mpya dhidi ya mashoga, akisema kuwa mara kwa mara Moscow imeonyesha mawazo ya vita baridi dhidi yake. 

Rais wa Marekani Barack Obama.
Rais wa Marekani Barack Obama. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwenye kipindi cha majadiliano Jumanne usiku, Obama amesema kuwa Moscow bado inatoa msaada nchini Afghanistan na katika lakini akazungumzia pia changamoto za msingi ambazo nchi yake imekuwa nazo pamoja na Urusi hivi karibuni.

Aidha rais Obama amemwambia rais wa Urusi Vladmir Putin kuwa asahau yaliyopita na kwa sasa wafikiri kuhusu wakati ujao na kwamba hakuna sababu za wao kushindwa kuendelea kushirikiana zaidi ya ilivyo sasa.

Obama amesisitiza kuwa angeweza kuhudhuria mkutano wa kilele wa G20 mwezi ujao huko Saint Petersburg, lakini hakusema kama angependa kukutana na Putin kwa ajili ya mazungumzo ya moja kwa moja jijini Moscow.

Aidha Obama amesema kuwa amesikitishwa na uamuzi wa Urusi kumpatia kibali cha mwaka mmoja kuishi nchini humo mfanyakazi wake wa zamani wa shirika la kijasusi Edward Snowden ambaye alivujisha taarifa za shirika hilo kwenye vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.