Pata taarifa kuu
SYRIA

Raisi wa Syria Bashar Al Assad ajihakikishia ushindi

Rais wa Syria, Bashar Al Assad, amekuwa akijiamini kushinda vita vya nchini mwake baada ya Vikosi vyake vya kijeshi kufanikiwa kurejesha kwenye himaya yake miji muhimu miwili iliyokuwa ikidhibitiwa na Waasi, huku mwenyewe akiamini kuwa atashinda vita dhidi ya Waasi.

Raisi wa Syria,Bashar Al Assad ambaye majeshi yake yanaendeleza mapambano dhidi ya makundi mbalimbali yanayopinga utawala wake nchini humo.
Raisi wa Syria,Bashar Al Assad ambaye majeshi yake yanaendeleza mapambano dhidi ya makundi mbalimbali yanayopinga utawala wake nchini humo. 路透瀾
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo baada ya kutangaza hatua hiyo, yalizuka mapambano makali mjini Homs kati ya Waasi na Vikosi vya Asad na kusababisha watu takriban 40 kupoteza maisha na kuwajeruhi wengine.

Akizungumza katika kuadhimisha siku ya Jeshi nchini humo Assad amewashukuru kwa kazi nzuri wanayoifanya akisema anawaamini hasa kwa kujiamini kwao katika kutekeleza na kuyafikia matazamio ya Syria kwa kupambana na makundi aliyoyaita ya kigaidi.

Brian Wanyama ni mchambuzi wa maswala ya kisiasa na mhadhiri toka chuo kikuu cha Masinde Muliro, Kakamega nchini Kenya anasema Assad anataka kuudhihirishia ulimwengu kuwa ni mshindi wa mapigano ya Syria.

Katika hatua nyingine Kiongozi wa Upinzani nchini humo, Burhan Ghaliun ameonesha kukerwa na kauli ya Assad, akisema kuwa ni upuzi kwa Kiongozi kutamka ushindi ilhali ameharibu nchi yake na kuua maelfu ya watu huku wengine akiwasababishia kukimbia makazi yao katika kipindi cha miaka miwili na nusu.

Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.