Pata taarifa kuu
URUSI-MAREKANI-SNOWDEN

Mahusiano ya Marekani na Urusi yaingia dosari baada ya Urusi kumpatia hifadhi Edward Snowden

Kitendo cha Urusi kumpatia hifadhi mfanyakazi wa zamani wa Shirika la kijasusi nchini Marekani, Edward Snowden,kimetia dosari uhusiano wa Marekani na Urusi, Wachambuzi wa mambo wameeleza.

Edward Snowden anatafutwa na Marekani kwa kuvujisha taarifa za siri juu ya miradi  ya siri  ya kijasusi ya Marekani
Edward Snowden anatafutwa na Marekani kwa kuvujisha taarifa za siri juu ya miradi ya siri ya kijasusi ya Marekani Reuters
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Rais wa Marekani,Barack Obama ilikuwa na matumaini ya kurejesha uhusiano uliokuwa ukiyumba, lakini Rais wa Urusi, Vladmir Putin ameelezwa kuwa amekuwa mgumu katika jitihada za kurejesha mahusiano mazuri.

Snowden anatafutwa na Marekani kwa kuvujisha taarifa za siri juu ya miradi ya siri ya kijasusi ya Marekani na alikuwa amekwama katika uwanja wa ndege wa jijini Moscow kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Urusi imekataa kumkabidhi Snowden kwa Marekani, zaidi, hapo jana Urusi ilimpatia Snowden hifadhi ya kipindi cha mwaka mmoja, hatua iliyoighadhabisha Marekani huku ikielezwa kuwa nchi hiyo imeharibu uhusiano ambao tayari ulikuwa na dosari juu ya tofauti za misimamo juu ya syria kati ya nchi hizo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.