Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI-URUSI-ISRAEL-UMOJA WA MATAIFA

Syria yaridhia kikosi cha Umoja wa mataifa kuchunguza matumizi ya silaha za kemikali

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wataelekea nchini Syria hivi karibuni kufanya uchunguzi katika maeneo matatu ambayo yameripotiwa kuwa kulikuwa na matumizi ya Silaha za kemikali, Umoja wa Mataifa umeeleza.

Raisi wa Siria Bashar Al Assad ambaye majeshi yake yanadaiwa kutumia silaha za kemikali kuwashambulia waasi huko Aleppo
Raisi wa Siria Bashar Al Assad ambaye majeshi yake yanadaiwa kutumia silaha za kemikali kuwashambulia waasi huko Aleppo 路透社
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Rais wa Syria, Bashar al Assad ilizuia kuingia kwa jopo la Wachunguzi tangu wito wa Umoja wa Mataifa ulipotolewa mwezi March kufanya uchunguzi juu ya silaha zilizopigwa marufuku.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano kufikiwa kati ya Wajumbe wawili wa umoja wa Mataifa walipokuwa nchini Syria kuzungumza na Serikali ya Syria,jijini Damascus juma lililopita.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa ripoti juu ya Matukio ya mashambulizi 13 ya kutumia silaha za kemikali iliwasilishwa, ushahidi ukitolewa na Syria, Uingereza, Ufaransa, Urusi na Marekani.

Tangazo la Umoja wa mataifa linakuja huku majeshi ya Raisi Bashar AL Assad yakianza mashambulizi huko Khan Al Asal jijini Aleppo ambapo hivi karibuni waasi waliweka ngome yao na ndipo mashambulizi ya silaha za kemikali yalipotekelezwa.

Msemaji wa umoja wa mataifa UN Martin Nersiky alibainisha kikosi cha upepelezi kinakuja kufuatia makubaliano ya ziara ya juma lililopita huko Damascus ziara iliyofanywa na Mkuu wa kitengo cha kusalimisha silaha Angela Kane na mkuu wa upelelezi wa silaha za kemikali Ake Sellstrom.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.