Pata taarifa kuu
DRC-M23-UN

MONUSCO yasikitishwa na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini DRCongo

Tume ya umoja wa mataifa nchini Jamuhri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ijulikanayo kama MONUSCO imesema inasikitishwa sana na ripoti zinazozidi kutolewa zikilaumu kundi la wapiganaji waasi wa M23 kuhusika na mauaji pamoja na kuwashikilia raia wasiokuwa na hatia.

REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

MONUSCO imesema Julai 24 mwaka huu waasi wa M23 waliendesha uporaji wa mali katika takribani nyumba 20 mjini Kiwanja mtaani Rutshuru ikiwa ni pamoja na kuwashikilia watu wasiopungua 40 baada ya kuwatuhumu kuchoma vituo vya kutoza kodi vya M23 katika mji huo uliopo Mashariki mwa DRCongo.

Aidha MONUSCO imesema tarehe 22 Julai waasi wa M23 waliwasajili watu 10 kwa nguvu mjini Kibumba mtaani Nyiragongo na kuwalazimisha kuchukua Silaha. Ripoti hiyo mebainisha kuwa watu watatu miongoni mwao waliuawa baada ya kujaribu kukimbia.

Wakati wa mapigano yaliyohusisha kundi la M23 na Jeshi la serikali ya Congo FARDC, waasi wa M23 walizuia magari ya mashirika ya kimataifa kupeleka misaada na kuwaokoa raia katika Mji wa Mutaho.

Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Abdallah Wafy amesema pamoja na jumla ya makosa hayo, waasi wa M23 watalazimika kujibu tuhuma hizo mbele ya dunia nzima.

Kwa upande wa M23 wamethibitisha kuwa zaidi ya watu 100 miongoni mwa wanaoshikiliwa katika gereza la Nyongera wameachwa huru.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema zaidi ya watu 200 walikamatwa na M23 alhamisi ya juma lililopita kufuatia tuhuma kwamba walishirikiana na wapiganaji Mai mai Nyatura.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.