Pata taarifa kuu
MAREKANI-MASHARIKI YA KATI

Waziri Kerry wa Marekani afaulu mpango wa kuendeleza mazungumzo ya amani Mashariki ya kati

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema kuwa mazungumzo ya amani baina ya Israeli na Palestina yaliyokwama kwa takribani siku tatu yanatarajiwa kuendelea mjini Washington juma lijalo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani  John Kerry
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry REUTERS/Mandel Ngan
Matangazo ya kibiashara

Baada ya siku moja iliyokuwa na utata mjini Ramalla kerry alitangaza mafanikio mapya ya kuzirejesha pande hizo mbili mezani tayari kwa mazungumzo.

Pande zote mbili za Israel na Palestina zilikuwa na mtazamo chanya isipokuwa kundi la kiislamu la Hammas ambalo limedhibiti ukanda wa gaza kupinga kurejea kwenye mazungumzo.

Tangazo la waziri kerry lilikuja baada ya kutumia siku nne kushawishi israel na palestina huko Amman ambapo baada ya kufanikiwa alizungumza na vyombo vya habari nchini humo.

Naye katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amewataka vingozi wa israel na palestina kuwajibika kuonyesha matumaini ya kuyaendeleza mazungumzo ya amani yaliyorejeshwa na marekani kwa lengo la kufanikisha amani ya mashariki ya kati.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.