Pata taarifa kuu
SYRIA

Mataifa ya Ghuba yatoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitisha mkutano wa dharura kuhusu Syria

Mataifa ya ghuba yametoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufanya mkutano wa dharura wa kuzuia mauaji katika mji wa Homs nchini Syria unaolengwa na mashambulizi makali ya wanajeshi wa serikali. 

Uharibifu katika mji wa Homs nchini Syria
Uharibifu katika mji wa Homs nchini Syria mobi.enca.com
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ya mataifa sita ya shirikisho la Ghuba wajumbe wa shirikisho hilo wametangaza kuwa wanaguswa sana na kutiwa wasiwasi na dhuluma na mashambulizi yasiyo ya haki yanayofanywa na vikosi vya serikali ya Syria kwenye mji wa Homs huku vikisaidiwa na wapiganaji wa kishia kutoka kundi la Hezbollah la nchini Lebanon chini ya mwamvuli wa kulinda mapinduzi ya Iran.

Mataifa hayo sita ya Ghuba Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Falme za Kiarabu na Saudi Arabia wamelitaka baraza la Usalama kufanya mkutano wa dharura ili kukomesha mauaji ya kutisha mjini Homs.

Mji wa Homs ambao unashikiliwa na waasi umekuwa shabaha mpya ya mashambulizi ya jeshi tangu siku ya Jumamosi.
Zaidi ya watu laki moja wanakadiriwa kuuawa katika mgogoro wa Syria hadi sasa, ambao ulizuka wakati wafuasi wa rais Assadwalipoanza mashambulizi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakipinga utawala wake mnamo March 2011.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.