Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-MANDELA-OBAMA

Rais wa Marekani Barack Obama akutana na familia ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela

Rais wa Marekani Barack Obama amekutana na familia ya mwasisi wa Taifa la Afrika Kusini Nelson Mandela, wakati huu ambapo shujaa huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi akiwa katika mapambano dhidi ya maradhi ya mapafu yaliyosababisha kuzorotesha afya yake.

REUTERS/Jason Reed
Matangazo ya kibiashara

Taarifa toka nchini humo zimeeleza kuwa Obama ameamua kutomtembelea shujaa huyo hospitalini anakopatiwa matibabu mjini Pretoria ili kudumisha amani na utulivu katika eneo hilo.

Obama amesema kuwa hakuwa na haja ya muda wa kupiga picha na Mandela kufuatia uvumi kwamba angeweza kumtembelea hospitalini kinara huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na mshindi mwenzie wa tuzo ya amani ya Nobeli ambaye amelazwa katika hospitalini kwa zaidi ya majuma matatu sasa.

Obama, ambaye alikutana Mandela mara moja jijini Washington mwaka 2005, amesema kuwa jambo la msingi kwake ni kumpa faraja Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini na ustawi wa familia yake.

Rais huyo wa marekani ameyazungumza hayo mjini Pretoria mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa sasa wa Afrika kusini, Jacob Zuma.

Ziara ya Rais Obama nchini Afrika Kusini haijawa na mvuto kama ilivyotarajiwa kutokana wananchi wa Taifa hilo kuelekeza zaidi macho na masikio yao katika maendeleo ya afya ya kiongozi wao wa zamani.

Wakati huo huo taarifa toka nchini humo zimearifu kuwa polisi wamelazimika kuwatawanya waandamanaji wanaopinga ziara ya kiongozi huyo maarufu duniani katika Taifa lao.

Ziara ya kiongozi huyo barani Afrika itatamatika nchini Tanzania na anatarajiwa kuwasili katika jiji la Dar es salaam siku ya jumatatu, Julai mosi 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.