Pata taarifa kuu
UN-BAN KI MOON

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa atowa wito wa mataifa mblimbali duniani kuwekeza zaidi kwa vijana

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa mataifa mbalimbali duniani kuwekeza zaidi kwa vijana ili kuwajengea uwezo wa kuibadilisha dunia kwa kuwa vijana ndiyo nguvu kazi inayotegemewa.

Katibu mkuu wa UN Ban Ki Moon
Katibu mkuu wa UN Ban Ki Moon
Matangazo ya kibiashara

Ban Ki Moon amesema kuwa hakuna maendeleo yatakayofikiwa kama dunia haitawashirikisha vijana ambao idadi yao kubwa ikilinganishwa na rika nyingine duniani.

Katibu mkuu huyo wa UN amefahamisha kuwa dunia inahitaji kutengeza ajira nusu bilioni katika miongo ijayo ili kutoa nafasi zaidi kwa vijana kwa lengo la kusukuma maendeleo ya kiuchumi.

Amesema vijana wanapaswa kuwezeshwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu na ujasiriamali. Ban pia alitowa mfano wa mwanamke kijana kutoka nchin Kenya ambaye alikulia katika makazi duni na kuanza mpango wa kazi na hatimaye kutowa ajira 500.

Ban Ki Moon alisema hii ilikuwa mfano wa jinsi ya ujasiriamali unaweza kubadilisha vijana wasio na ajira na kuwa waajiri, lakini pia kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya maendeleo endelevu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.