Pata taarifa kuu
URUSI-MAREKANI

Marekani na Urusi zavutana juu ya Erdowan, afisaa huyo wa zamani wa CIA anaye daiwa kukimbilia nchini Urusi

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ameitolea wito serikali ya Marekani kuonyesha ushirikiano wake kwa kumrejesha nchini Marekani Edward Snowden anaetafutwa na taifa hilo kwa kosa la uhaini, na kudai kuwa serikali ya Washington haitaki mzozano wowote kuhusu swala hilo.

Sergei Lavrov, waziri wa mambo ya nje wa Urusi
Sergei Lavrov, waziri wa mambo ya nje wa Urusi
Matangazo ya kibiashara

Akiwa ziarani nchini Saudia Arabia, John Kerry amesema kwamba kurejeshwa nchini Marekani kwa afisa huyo wa zamani wa Idara ya Ujasusi ya Marekani CIA na Idara ya Usalama NSA, ni swala la kuheshimu sheria.

Hata hivyo serikali ya Urusi imesema afisa huyo wa zamani wa CIA hajakanyaga nchini humo, na kutupilia mbali madai ya serikali ya Marekani kwamba yupo nchini Urusi. serikali hiyo imeendelea kuituhumu Marekani kuhusika katika kutoroka kwa afiasa huyo.

Inadaiwa kuwa Snowden aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Sheremetyevo jijini Moscou katika ndege iliokuwa ikitokea jijini Hong Hong siku ya Jumapili. Viongozi wa Urusi wao wanasisitiza kuwa afisa huyo hakutoka ndani ya ndege.

Hali inakuja kuhatarisha mvutano baina ya Urusi na Marekani, pamoja na China wakati mataifa hayo yakiangalia kijicho kibaya kwa kushindwa kuafikiana juu ya vita vinavyoendelea nchini Syria.

akizungumza na vyombo vya habari waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema hawahusika kamwe na safari za Snowden na uhusinao wake na vyombo vya sheria nchini Marekeni.

Hata hivyo waziri Lavrov hakukanusha aidha kuthibitisha kuwa afisa huyo wa zamani wa idara ya ujasusi nchini Marekani CIA na mataalamu wa idara ya Usalama NSA aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Sheremetyevo juzi Jumapili, bali amesisitiza kuwa  Snowden hajakanyaga ardhi ya Urusi na hakutoka kwenye Uwanja wa ndege.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.