Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-ECUADOR

Marekani yasema itatumia njia zote za kisheria kuhakikisha inamtia nguvuni Edward Snowden

Edward Snowden mfanyakazi wa zamani wa idara ya ujasusi nchini Marekani ambaye anatafutwa na taifa hilo kwa kosa la uhaini baada ya kutowa taarifa za siri juu ya mpango wa Marekani kuhusu uchunguzi wa matumizi ya mawasiliano ya ki elektroniki, hadi sasa haijulikani alipo, licha ya duru nyingi kuendelea kutaja kuwa bado yupo nchini Urusi.

Barack Obama na Edward Snowden
Barack Obama na Edward Snowden REUTERS/Bobby Yip
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi Vladimir Poutine ambaye yupo kimya hadi leo kuhusu swala hilo la Snowden, huenda akalizungumzia wakati wa ziara yake katika jiji la Turku nchini Finlande ambako anataraji kufanya mkutano na vyombo vya habari.

Rais wa Marekani Barack Obama amesema serikali yake itatumia njai zote za kisheria kuhakikisha imemtia nguvuni mfanyakazi huyo wa zamani wa CIA.

Hapo jana kulikuwa na taarifa kwamba Snowden yupo nchini Urusi ambapo Serikali ya Marekani iliomba Moscou kushirikiana nayo katika shughuli za kumsafirisha nchini Marekani mfanyakazi wa zamani wa kituo cha intelijensia cha Marekani CIA Edward Snowden ili kujibu tuhuma dhidi yake.

Msemaji wa usalama wa taifa nchini Marekani caitlin Hayden amefahamisha kuwa kutokana na ushirikiano wa mataifa hayo mawili ulioimarika tangu kutokea kwa mlipuko jijini Boston wakati wa mbio za Marathon, Pamoja na utekelezwaji wa usafirishaji wa wahalifu wakuu, kuna matumaini makubwa kuona serikali ya Urusi inamfukuza Edward Snowden nchini Marekani ili akapambane na mahakama.

Msemaji huyo wa idara ya usalama nchini Marekani amesema kusiktishwa na hatuwa ya serikali ya Hong kong ya kumuacha Snowden kuelekea nchini Moscou licha ya ombi halali la Marekani la kutaka kukamatwa kwake kama unavyoruhusu mkataba wa ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili.

Hayden amesema wamewasilisha ujumbe wa lamawa kwa Hong kong na serikali ya China kupitia njia za kidiplomasia na kufahamisha kuwa uamuzi kama huo unaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa uhusiano uliopo kati ya Marekani na Hong Kong na Marekani na China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.