Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-MANDELA

Serikali ya Jacob Zuma yakiri kuwa hali ya Mandela ni mbaya sana

Rais wa Afrika Kusini amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kukiri kuwa hali ya rais wa zamani wa taifa hilo ni mbaya, ma dactari wanaendelea kufanya kila jitihada kuhakikisha kiongozi huyo wa zamani kinara wa ubaguzi wa rangi anaye sumbuliwa na maradhi ya mapafu, anapata nafuu. wananchi wa taifa hilo la dunia nzima wametolewa wito wa kumuombea.

Nelson Mandela
Nelson Mandela
Matangazo ya kibiashara

Akizungumzia kuhusu hali ya afya ya Mandela Rais Zuma alifahamisha kuwa hapo jana akiw ana makam mwenyekiti wa chama cha ANC chama madarakani Cyril Ramaphosa na Graça Machel mke wa Nelson Mandela, wamekutana jana Jumapili ili kuzungumzia hali hiyo.

Zuma amesema ma dactari wanamtibu kinara huyo wa zamani wa ubaguzi wa rangi wanafanya kila jitihada ili kuboresha hali yake ya afya.

Ikulu ya Marekani hapo jana ilifahamisha kwamba fikra na sala na maombi zinaelekezwa kwa Nelson Mandela baada ya kupata habari ya kuzorota kwa afya yake, wakati rais Barack Obama akiandaa ziara barani Afrika ikiwemo Afrika Kusini.

Kulikuwepo na ukimya wa takriban juma moja ambapo Jumamosi juma lililopita ikulu ya rais iliarifu kuwa hali ya afya ya Nelson Mandela ni mbaya lakini tulivu, lakini baadae kituo cha televisheni cha Marekani cha CBS kiliarifu kuwa hali ya afya ya Kinara huyo ni mbaya zaidi kuliko inavyo fikiriwa.

Taarifa ya mwisho ilitolewa na rais wa taifa hilo Juni 16 na kuarifu kuwa hali yake inaendelea vizuri

kwa mujibu wa kituo hicho cha CBS rais huyo wa zamani alitakiwa kutiliwa vifaa vya kuhamasisha mwili tangu pale alipo lazwa Hospitalini, kwani ini na figo zake vilikuwa vinafanya kazi kwa asilimia hamsini, lakini tangu siku mbili hajafungua macho.

Taarifa hiyo, ya kituo cha CBS ilikanushwa vikali na mtoto wa kwanza wa rais Mandela Makaziwe Mandela ambaye alifahamisha kwamba anafungua macho.

Ikulu ya rais nchini Afrika Kusini imeendelea kufahamisha kwamba gari ya kubebea wagonjwa iliokuwa ikimsafirisha Hospitalini Kinara huyo wa ubaguzi wa rangi Juni 8, ambayo iliharibika njiani kwa muda wa dakika arobaini haikusababisha hali hiyo kudhorota zaidi.

Hali ya wasiwasi ilikuwa imetanda katika siku za nyuma wakati alipolazwa kinara huyo, na baadae matumaini kurejea baada ya rais Zuma kufahamisha kwamba hali yake inaendelea kuimarika.

Asilimia kubwa ya wajumbe wa vyombo vya habari waliotumwa huko nchini Afrika Kusini vilirejea nyumbani huku ikianza kutolewa taarifa ya kuondoka Hospitalini kwa rais huyo wa zamai wa Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.