Pata taarifa kuu
UTURUKI

Erdogan atoa onyo la mwisho kwa waandamanaji kuacha maandamano

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa onyo la mwisho kwa maelfu ya waandamanaji kuacha kuandamana dhidi ya serikali na kuondoka jijini Istanbul au watakiona cha mtema kuni.

Matangazo ya kibiashara

Erdogan ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha kuwa wanaowaondoa watoto wao katika viwanja vya Gezi ambavyo  waandamanaji hao wamekuwa wakiandama kwa wiki mbili sasa dhidi ya serikali ya Erdogan.

Onyo hili linakuja siku moja baada Erdogan kusema kuwa huenda akalazimika kutangaza kufanyika kwa kura ya maoni nchini humo  kuamua hatima ya maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali jijini Instabul na miji mingine nchini humo.

Chama cha siasa cha AK kinasema kuwa kipo tayari kwa kura ya maoni kuamua mustakabali wa maandamano hayo pamoja na serikali ya Waziri Mkuu Erdogan.

Licha ya hali ya utulivu kushuhudiwa kwa saa kadhaa siku ya Jumatano, waandamanaji walijitokeza tena katika ukumbi wa Taksim na kuanza kukimbiza na polisi waliotumia mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratisha.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu likiweno lile la Kimataifa la Amnesty International limemshtumu nguvu inayotumiwa na polisi dhidi ya maandamano hayo na badala yake inataka serikali kuzungumza na waandamanaji hao.

Waandamanaji hao wanasema wamechoswa na serikali ya Erdogan na pia wanaongeza kuwa kiongozi huyo ameanza kuweka sheria za Kislamu nchini humo kinyume na sheria.

Erdogan alikutana na baadhi ya viongozi wa makundi ya waandamanaji siku ya Jumatano  kuzungumzia maandamano hayo huku waandamanaji wengine wakisema waliokwenda katika mazungumzo hayo hawakuwa viongozi halisin waliokuwa wanawaakilisha.

Juma lililopita Erdogan aliwaambia wafuasi wake kuwa wamekuwa wavumilivu mno na mwishoni mwa wiki hii nao wataanza mikutano yao ya hadhara ya kuiunga mkono serikali ikiwa maandamnao ya wapinzani yataendelea.

Maandamano nchini Uturuki yalianza mwisho mwa mwezi uliopita jijini Instabul na kusambaa kote nchini kupinga uongozi wa Erdogan ambao waandamanaji hao wanasema ni wa Kidikteta.

Waandamanaji zaidi ya 5,000 wamejeruhiwa kutokana na maandamano hayo wengi wao vijana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.