Pata taarifa kuu
ULAYA

Watu 10 wahofiwa kupoteza maisha kutokana na mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa kuzikumba nchi za Ulaya ya Kati

Watu wanaokadiriwa kufikia kumi wamepoteza maisha Barani Ulaya kutokana na mafuriko yanayoendelea kuongeza hofu katika Ulaya ya Kati na kuleta hofu katika nchi za Ujerumani, Austria, Uswiss na Jamhuri ya Czech.

Mafuriko ambayo yamezingira miji kadhaa Barani Ulaya yanayosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha
Mafuriko ambayo yamezingira miji kadhaa Barani Ulaya yanayosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha
Matangazo ya kibiashara

Mafuriko hayo yamezua hali ya taharuki katika nchi zinazopatikana Ulaya ya Kati kwani nchi hizo zimeshuhudia shughuli nyingi zikilazimika kufungwa kutokana na ongezeko kubwa la maji linalozikumba nchi hizo.

Mji Mkuu wa Jamhuri ya Czech, Prague ndiyo unatajwa kuathirika zaidi ukilinganisha na sehemu nyingine kutokana na maji hayo kusafiri kwa kasi ya kilometa 30 kwa saa na kuleta madhara zaidi.

Hali imezidi kuwa mbaya nchini Jamhuri ya Czech kutokana na kingo za Mto Elbe kupasuka na hivyo kuchangia maji kusambaa zaidi na sasa yameanza kuleta madhara katika mpaka wake na Ujerumani.

Msemaji wa Kitengo cha Utabiri wa Hali ya Hewa nchini Jamhuri ya Czech Petr Dvorak amekiri hali inaweza kuwa mbaya zaidi iwapo mvua zinazonyesha hazitakoma kwa sasa kwani zitasababisha maji zaidi kujaa.

Jeshi la Polisi nchini Jamhuri ya Czech kupitia Msemaji wake Pavla Kopecka limethibitisha kutokea kwa vifo katika nchi hiyo huku mtu aliyepoteza maisha hivi karibuni akiwa mwanamke aliyeangukiwa na mti akifanya juhudi za kumuokoa mbwa wake.

Takwimu zinaonesha watu wawili wamepoteza maisha nchini Austria tangu kuanza kwa mafuriko hayo huku nchini ya Uswiss ikipoteza mtu mmoja lakini hakuna taarifa ya kifo nchini Ujerumani.

Ujerumani kwa upande wake inaendelea kuchukua hatua zaidi kuhakikisha inakabiliana na mafuriko hayo ambayo yamechangia hata kukatisha mawasiliano ikiwemo ya barabara kutokana na baadhi yao kukatika.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametoa ahadi ya kuwasaidia waathirika ambapo tayari wameshatenga dola milioni 130 kwa ajili ya tahadhari kuzuia madhara zaidi yanayosababishwa na mafuriko hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.