Pata taarifa kuu
COLOMBIA

Rais wa Colombia Juan Santos asikitishwa na kitisho cha kuuawa kwa Kiongozi wa FARC akihofia kutavunja mazungumzo ya amani

Serikali ya Colombia imesikitishwa na hatua ya kutumwa kwa kitisho cha kifo kwa Kiongozi wa Muungano wa Kundi la Waasi la FARC ambalo linaendelea kufanya mazungumzo na serikali kumaliza mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miongo mitano.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ambaye anahofia vitisho vya kuuawa kwa Viongozi wa FARC kunaweza kukazorotesha mazungumzo ya amani
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ambaye anahofia vitisho vya kuuawa kwa Viongozi wa FARC kunaweza kukazorotesha mazungumzo ya amani REUTERS/John Vizcaino
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos amesema taarifa hiyo ya kitisho kwa Kiongozi wa FARC itachangia pakubwa kuzorotesha mazungumao ya amani ambato yameanza na kupiga hatua.

Rais Santos ameonekana kukerwa na hatua hiyo ya kupelekwa vitisho kwa Viongozi wa FARC akiamini wakijitoa kwenye mazungumzo hayo nchi hiyo itarudi nyuma na kushindwa kufikia malengo yake ya kumaliza mapigano na kundi hilo.

Kiongozi huyo wa Colombia ametoa wito kwa FARC kupuuza taarifa hiyo ya vitisho vya vifo kwa Viongozi wake na badala yake waendelee na mazungumzo ya amani ambayo yatasaidia kurejesha utulivu nchini humo.

Serikali ya Colombia ipo kwenye mazungumzo ya amani na Kundi la Waasi la FARC ambapo masuala sita ndiyo yamekuwa yakijadili kuhakikisha hali ya utulivu inarejea baada ya kukosekana kwa zaidi ya miongo mitano.

Tayari Serikali ya Colombia na Waasi wa FARC wamekubaliana kwenye suala la mabadiliko ya ardhi ambapo kumekuwa na maafikiano ya kuhakikisha wale walioporwa wanalipwa fidia kutokana na kupoteza ardhi yao.

Mambo mengine ambayo yanaendelewa kujadili kwa pamoja na pande hizo mbili ni suala la ushiriki kwenye siasa, kusalimisha silaha, kupambana na dawa za kulevya, kutambuliwa haki za waathirika sambamba na utekeleza wa makubaliano ya amani.

Iwapo pande hizo mbili zitaafikiana kwenye masuala hayo matano yaliyosalia huenda nchi ya Colombia ikashuhudia hali ya utulivu ikarejea baada ya wananchi wake kuwa katika hofu ya usalama kwa miongo mitano.

Rais Santos ametoa wito wa kuhakikisha pande zote zinaweka maslahi ya Taifa mbele kitu kitakachosaidia pakubwa kufanikiwa kwa mazungumzo hayo na hatimaye utulivu kurejea nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.