Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SUDAN-MISRI

Ethiopia yaanza ujenzi wa bwawa lililozusha utata, Misri na Sudan zakashifu mradi huo

Nchi ya Ethiopia imeanza mpango wake wa kubadilisha mwelekeo wa maji ya mto Blue Nile kwa lengo la kujenga bwawa kubwa la kuzalisha nguvu za umeme, hatua iliyoibusha hofu kwa mataifa jirani yanayotumia maji ya mto Nile.

Mchoro unaonesha namna bwawa la kuzalisha nguvu za Umeme la Ethiopia utakapokamilika
Mchoro unaonesha namna bwawa la kuzalisha nguvu za Umeme la Ethiopia utakapokamilika Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mpango huo wa Ethiopia kuanza kutumia maji ya mto Blue Nile kwa matumizi ya kuzalisha umeme umezua hofu ya kupungua kwa maji kwenye nchi za Misri na Sudan ambazo zimeonya kuhusu mpango wa Ethiopia.

Hapo jana Serikali ilifanya sherehe maalumu za ufunguzi wa ujenzi wa bwawa hilo ambalo maji yake yatakuwa yakitumika kuzalisha nguvu za umeme utakaotumika kuchochea maendeleo ya taifa hilo ambalo lina upungufu mkubwa nishati hiyo.

Waziri wa nishati nchini Ethiopia, Demeky Mekonin akifungua mradi wa ujenzi wa bwawa hilo amesema likikamilika litakuwa ni mkombozi mkubwa kwa nchi yao na kwamba sasa kila mwananchi atakuwa na uhakika wa kusambaziwa nishati ya umeme.

Waziri Mekonin ameongeza kuwa ujenzi wa bwawa hilo ukikamilika utakuwa na manufaa sio tu kwa nchi ya Ethiopia lakini hata nchi jirani zitanufaika kwa kuwa zitakuwa na uwezo wa kununua umeme toka nchini humo.

Nchi za Sudan na Misri zinapinga ujenzi huo zikisema unakiuka makubaliano yaliyotiwa siani wakati wa ukoloni mkataba unaipa haki nchi ya Misri kumiliki asilimia 70 ya sehemu ya mto Nile.

Serikali ya Ethiopia inasema Misri haitaathirika na ujenzi wa bwawa hilo kwakuwa mkataba wa mwaka 1959 haukuzingatia nchi nyingine tano ambazo zinatumia maji ya mto Nile.

Ujenzi wa bwawa hilo unatarajiwa kuigharimu nchi ya Ethiopia zaidi ya dola Bilioni 5 hadi 6 na ukikamilika litazalisha megawati elfu sita za umeme.

Bwawa hilo linaelezwa kuwa kubwa zaidi kuwahi kujengwa barani Afrika na kufadhiliwa na fedha za serikali baada ya wafadhili wa kigeni kukataa kutoa fedha zao kutokana na mzozo uliopo wa matumizi ya maji ya Mto Nile.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.