Pata taarifa kuu
IRAQ

Mashambulizi ya kujitoa muhanga yaua watu zaidi ya 58 nchini Iraq

Mashambulizi ya mabomu mjini Baghdad na kaskazini mwa nchi ya Iraq yameua watu zaidi ya 58 na kujeruhi wengine mamia ikiwa ni mfululizo wa machafuko ya kidini yaliyoibuka hivi karibuni nchini humo.

Moja ya mashambulizi ya mabomu yaliyotekelezwa hivi karibuni mjini Baghdad Iraq
Moja ya mashambulizi ya mabomu yaliyotekelezwa hivi karibuni mjini Baghdad Iraq Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi yaliyotekelezwa mjini Baghdad yalilenga raia wa jamii ya Kishia ambao wamekuwa wakilengwa na watu wa jamii ya Sunni kwenye vurugu ambazo Serikali imeonya kuhusu kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mashambulizi haya yanaongezeka kufuatia jamii ya Sunni ambayo ina watu wachache nchini Iraq kuwatuhumu watu wa jamii ya Kishia ambao ndio wanaoongoza Serikali kwa madai kuwa wamekuwa wakinyimwa haki zao.

Takwimu zilizotolewa na Serikali zinaonesha kuwa zaidi ya watu elfu moja wamekwisha uawa ndani ya miezi miwili pekee kutokana na mashambulizi ya mabomu ya kujitoa muhanga baina ya jamii hizo mbili.

Hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na mashambulizi ya kuamkia leo ingawa kundi la jamii ya Sunni lenye uhusiano na mtandao wa kigaidi duniani wa Al-qaeda wanatajwa kuhusika na kupanga njama za kutekeleza mashambulizi hayo.

Hofu ya kiusalama imeendelea kutanda nchini Iraq wakati huu mashambulizi hayo yakiongezeka ambapo serikali ya waziri mkuu Nuru al-Maliki imeagiza kuimarishwa kwa usalama kwenye maeneo mengi ya nchi.

Toka kuondoka nchini humo kwa vikosi vya Marekani na washirika wake, kumeripotiwa mashambulizi kuongezeka na kuzusha maswali kuhusu uimara wa wanajeshi wa Serikali ambao wameachiwa kutoa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.