Pata taarifa kuu
CHINA-INDIA

India na China zaapa kutatua mzozo wa mpaka baina yake

Mawaziri wakuu wa India na China wameapa kutatua mgogoro wa mpaka ambao umechachusha mahusiano baina ya nchi hizo mbili kwa miongo kadhaa, wakisema kuwa mahusiano mazuri kati ya mataifa hayo makubwa barani Asia ni muhimu kwa amani ya dunia. 

Waziri mkuu wa China Li Keqiang akiwa na waziri mkuu wa India Manmohan Singh
Waziri mkuu wa China Li Keqiang akiwa na waziri mkuu wa India Manmohan Singh deccanchronicle.com
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, akiwa katika ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu aingie madarakani, amesema kwamba Beijing imedhamiria kujenga uaminifu na New Delhi wakati yeye na timu ya mawaziri wakitia saini mfululizo wa makubaliano ya pamoja na India.

Mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh, pia amesisitiza kuwa uhusiano mzuri baina ya nchi hizo ni muhimu kwa maendeleo ya ukanda mzima.
 

Ziara hii imekuja ikiwa yamepita majuma kadhaa toka kushuhudiwa makabiliano kati ya wanajeshi wa India na China kwenye eneo la mpaka wa Kashimir Mashariki mwa nchi hiyo.

Li Keqiang amekuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, waziri mkuu, Manmohan Singh mazungumzo ambayo mbali na kujadili suala la usalama kwenye eneo la milima ya Himalaya, pia wamejadili uhusiano wa kibisahara kati ya mataifa hayo mawili.

Baadhi ya wanaharakati nchini India wamekosoa ziara hiyo kwa kile walichodai ni serikali ya India kushindwa kuweka sheria kudhibiti uwekezaji unaofanywa na raia wa China ambao wanachukua ajira za wenyeji pamoja na kugombea eneo la mpaka wake.

Waziri mkuu,Li Keqiang mbali na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Manmohan Singh, atakutana na waziri wa mambo ya nje wa India Salman Khurshid, na viongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini India cha BJP.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.