Pata taarifa kuu
ICC-MAREKANI-RWANDA

Marekani yajiandaa kumsafirisha Bosco Ntaganda Hague

Marekani inasema Ubalozi wake mjini Kigali nchini Rwanda unajiandaa kumsafirisha Jenerali Bosco Ntaganda aliyejisalimisha kwenye ubalozi wake  na kwamba wana matumaini kupata ushirikiano toka kwa serikali ya Rwanda.

Matangazo ya kibiashara

Bosco Ntaganda aliishangaza dunia juma hili baada ya kujisalimisha mwenyewe kwenye ubalozi wa Marekani nchini Rwanda akitaka msaada wa kufikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

Msemaji wa kundi la M 23 linalowakilishwa na Askofu Jean Marie Runiga, Salomon Baravuga amesema kiongozi wake ndiye aliyemshawishi Ntaganda kujisalimisha huku akikanusha kundi lake kuwa na uhusiano na kiongozi huyo.

Kwa upande mwingine msemaji wa kisiasa wa kundi la M23 linaloongozwa na Sultan makenga, Betrand Bisimwa ameendelea kusisitiza kuwa Runiga na kundi lake walikuwa na uhusiano wa karibu na Ntaganda waliyetaka arejee katika kundi lao.

Rais Joseph Kabila ameendelea kukutana na viongozi mbalimbali nchini humo kujadili hali ya amani Mashariki mwa nchi hiyo huku baada ya Ntaganda kujisalimisha.

Ntaganda anatuhumiwa kuongoza makundi kadhaa ya uasi Mashariki mwa nchi hiyo kabla ya kupewa cheo katika jeshi la serikali kaa njiamojawapo ya kuleta amani Mashariki mwa nchi hiyo.

Aidha, ametuhumiwa kuongoza kundi la waasi la M 23 kulipa silaha ili kukabiliana na serikali ya Kinsasha huku akitihumiwa na Mahakama ya ICC kutekeleza visa vya ukiuwkaji wa haki za bindamu ikiwemo kuwaajiri watoto wadogo katika jeshi lake na pia kutekeleza mauji na ubakaji wa wanawake.

Ofisi ya kiongozi wa Mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC mjini Hague imesema kuwa inawasiliana na serikali ya Rwanda pamoja na Marekani kuhakikisha kuwa Ntaganda anafika Hague ili kufunguliwa mashtaka yanayomkabili.

Mahakama hiyo ya ICC imeongeza kuwa kujisalimisha kwa Ntaganda ni habari njema kwa raia wote wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao wameteseka mikononi mwa kiongozi huyo wa kundi la waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.