Pata taarifa kuu
Iraq

Watu zaidi ya 50 wauawa mjini Baghdad nchini Iraq baada ya mashambulizi ya bomu

Mashambulizi zaidi ya 20 ya bomu yametikisa mji wa Baghdad nchini Iraq na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 50 siku moja kabla ya kuadhimisha miaka 10 tangu Marekani ilipondoa wanajeshi wake nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya 170 wamejeruhiwa baada ya kutokea kwa mashambulizi hayo yanayoelezwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo ndani ya miezi sita iliyopita .

Mashambulizi mengi yametokea katika maeneo yenye wakaazi wengi wa Kishia, mjini Baghdad na kusababisha barabara kuu kufungwa mjini humo.

Mwezi Septemba  mwaka uliopita, mashambulizi mengine kama hayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 76 na mamia kujeruhiwa.

Tarehe 20 mwezi wa Machi mwaka 2003 majeshi ya Marekani yaliondoka Iraq baada ya kutangaza kuwa oparesheni yao ilikuwa imekamilika.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakituhumu oparesheni hiyo iliyosababisha mauaji ya zaidi ya watu laki moja  baada ya wanajeshi hao kuondoka nchini humo.

Serikali ya Iraq bado haijatangaza ikiwa itaadhimisha miaka kumi tangu wanajeshi wa Marekani walipoondika nchini humo.

Baraza la Mawaziri nchini humo limesema kuwa kutokanana sababu za kiusalama Uchaguzi Mkuu wa tarehe 20 mwezi Aprili huenda usifanyike kama ilivyopangwa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.