Pata taarifa kuu
DR Congo-Rwanda

Waasi wa M23 wakimbilia Rwanda,wasalimisha silaha

Wapiganaji wa kundi la waasi wa M23 la nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo wamekimbilia nchi jirani ya Rwanda baada ya mapigano makali kati yao na wapinzani wao kutoka kundi la Sultan Makenga.

Baadhi ya wapiganaji wa Kundi la waasi wa M23 wamekimbilia nchini Rwanda baada ya mapambano makali kati yao na waasi watiifu wa Sultan Makenga
Baadhi ya wapiganaji wa Kundi la waasi wa M23 wamekimbilia nchini Rwanda baada ya mapambano makali kati yao na waasi watiifu wa Sultan Makenga REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya kigeni nchini Rwanda Louise Mushikiwabo amethibitisha kwamba takribani wapiganaji mia sita walikuwa miongoni mwa watu waliovuka mpaka wa Rwanda na kuingia nchini humo siku ya ijumaa na mapema jumamosi wakitokea eneo lenye machafuko nchini jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Taarifa zimebainisha kuwa wapiganaji hao waasi kutoka nchini DR Congo wamenyang'anywa silaha na kuwekwa kizuizini huku baadhi wakitibiwa majeraha na shirika la msalaba mwekundu.

Miongoni mwa wapiganaji hao alikuwepo kiongozi wa zamani wa kundi la m23 Jean-Marie Runiga, ambaye kikundi chake kimekuwa kikipigana na wapinzani wake ambao ni askari watiifu wa kundi la kijeshi,linaloongozwa na Sultani Makenga, tangu Machi 9.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.