Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Shahidi wa Kwanza wa kesi ya Mwanariadha Oscar Pistorius akiri kusikika kwa sauti kubwa kabla ya kuuwa kwa Reeva

Mwanariadha mwenye ulemavu wa miguu nchini Afrika Kusini na mshindi wa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki Oscar Pistorius ameendelea kugongwa mwamba kupata dhamana kwa mara nyingine huku kesi ikionekana kumuendea vibaya. Pistorius ambaye anatuhumiwa kwa mauaji ya Mpenzi wake ambaye ni Mwanamitindo Reeva Steenkamp amepanda kizimbani kwa mara nyingine hii leo huku shahidi wa kwanza akianza kutoa ushahidi unaoanza kumkandamiza mwanariadha huyo.

Mwanariadha Oscar Pistorius akiwa mbele ya Mahakama ya Pretoira kusikiliza kesi ya mauaji inayomkabili
Mwanariadha Oscar Pistorius akiwa mbele ya Mahakama ya Pretoira kusikiliza kesi ya mauaji inayomkabili REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Pretoria ilianza kumsikiliza shahidi wa kwanza ambaye ameeleza ilisikika sauti kubwa kutoka nyumbani kwa Pistorius kabla ya Mpenzi wake Reeva hajapigwa risasi nne na kupoteza maisha.

Shahidi huyo wa kwanza ambaye ni Hilton Botha baada ya kueleza kile ambacho amekisikia upande wa uetetezi ukambana kwa maswali mengi lakini akaendelea kushikilia msimamo wake wa kusikika kwa sauti hiyo kubwa.

Pistorius alipanda kizimbani kwa mara ya pili hii leo huku akionekana mwenye mawazo na mpole na akisikiliza kwa makini ushahidi ambao ulikuwa unatolewa dhidi yake kwenye kesi ya mauaji inayomkabili.

Mahakama imeelezwa risasi tatu ndiyo zilimpata Reeva ambazo zilitua sehemu za mwili wake ikiwa ni kichwani, kwenye kiwiko na kwenye paja kitu ambacho kisababisha damu nyingi kutoka.

Botha kwenye ushahidi wake naye ameendelea kusisitiza maneno ambayo yalitolewa na Mwendesha Mashtaka ya kwamba risasi hizo zilifyatuliwa kupitia mlango wa bafuni na kumpata Mwanamitindo huyo.

Shahidi huyo alikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza kufika eneo la tukio na kumkuta Reeva ameshafikwa na mauti baada ya kupigwa risasi hizo tatu zilizoingia mwilini mwake na Mpenzi wake Pistorius.

Mahakama imekataa kutoa dhamana kwa Pistorius kutokana na kuogopa hatari iliyombele yake kutokana na wananchi wengi kwa sasa kuendelea kuwa na hasira na wanaweza wakamfanyia kitu chochote kibaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.