Pata taarifa kuu
SYRIA

Pande zinazohasimiana nchini Syria zote zatuhumiwa kutenda Uhalifu wa Kivita dhidi ya Binadamu kwa kipindi cha miezi 23

Umoja wa Mataifa UN umezilaumu pande zinazohasimiana nchini Syria kwamba zote zimehusika na uhalifu wa kivita kutokana na kushiriki kwenye mapigano yaliyochangia mauaji kwa kipindi cha miezi 23. Tamko hilo la kuzishutumu pande zote zinazohusika kwenye mgogoro wa Syria kutenda makosa ya uhalifu wa kivita limetolewa na Tume Maalum ya Umoja wa Mataifa Inayochunguza makosa yaliyofanywa.

Athari ambazo zimetokana na mapigano yanayoendelea nchini Syria yakihusisha serikali na upinzani
Athari ambazo zimetokana na mapigano yanayoendelea nchini Syria yakihusisha serikali na upinzani REUTERS/Mahmoud Hassano
Matangazo ya kibiashara

Tume Ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa UN inaongozwa na Paulo Sergio Pinheiro raia wa Brazil na imelitaka Baraza la Usalama la Umoja huo kuhakikisha linachukua hatua za haraka kukabiliana na uhalifu huo wa kivita.

Carla del Ponte ni Mwendesha Mashtaka wa zamani wa Umoja wa Mataifa UN na Mjumbe kwenye Tume amesema wamependekeza Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC ihusike kwenye hili.

Mjumbe huyo wa Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa UN amesema wao hawana uamuzi wa mwisho juu ya nini kifanyike lakini wataendelea kuishinikiza Jumuiya ya Kimataofa kuchukua hatua kwa wakati.

Del Ponte ametoa kauli hiyo baada ya kutoa ripoti ya uchunguzi wao mbele ya waandishi wa habari na kusema kazi yao ilikuwa kufanya uchunguzi na hivyo sasa wangependa Mahakama ya ICC ikapewa nafasi kufanya kazi yao.

Ripoti hiyo inaonesha pande zote zimehusika kwenye ubakaji na mauajia ya wananchi wasio na hatia kayika kipindi chote cha miezi 23 na hivyo wanastahili kukabiliwa na mkono wa sheria kwa makosa ya uhalifu wa kivita.

Tume ya Uchunguzi imeamua kulipeleka suala hilo kwa Mahakama ya ICC kutokana na Baraza la Usalama kugawanyika kila mara juu ya hatua za kuchukua katika kumaliza umwagaji wa damu huko Syria.

Majeshi tiifu kwa Rais Bashar Al Assad yameendelea kukabiliana vilivyo na Wapinzani na kuchangia vifo vya watu ambao wanazidi 60,000 katika Taifa la Syria kitu ambacho kinaonekana kuwa kitisho kwa hatima ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.