Pata taarifa kuu
DR Congo

Upinzani nchini DR Congo kuhamasisha maandamano dhidi ya Raisi Joseph Kabila

Upinzani nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo umetangza maandamano mjini Kinshasa jumamosi hii kupinga utawala wa rais Joseph Kabila licha ya kupigwa marufuku.

Raisi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila
Raisi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila rfi
Matangazo ya kibiashara

Chama cha FAC ambacho kina jumla ya wabunge 8 katika bunge la DR Congo kimebainisha kuwa hali inazidi kuwa mbaya kila uchao nchini humo na hivyo kumtaka raisi kabila kujiuzulu kwa vile kuna kila dalili kuwa kashindwa kuiongoza vema nchi hiyo.

Aidha Chama hicho kimeutuhumu utawala wa raisi kabila kujaa mapungufu ambayo yameendelea kuizorotesha hali ya usalama wa taifa hilo tangu alipochaguliwa kwa mara nyingine kuiongoza Congo.

Hali ya amani mashariki mwa DR Congo bado ni kitendawili kufuatia uhalifu unaoendeshwa na waasi wakiwemo wa kundi la M23 na kusababisha wakazi kuyakimbia makazi yao na kutofanya shughuli za uzalishaji mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.