Pata taarifa kuu
Mali-Ufaransa

Wapiganaji wa kundi la DJihad waondoka katika miji ya kaskazini wakati majeshi ya Ufaransa yakiwasili nchini Mali

Wapiganaji wa kundi la Djihad wameondoka katika miji ya Timbuktu, Gao na Duenza  kaskazini mwa Mali baada ya kukabiliwa na mashambulizi makali ya anga yanayoendeshwa na ndege za kijeshi za Ufaransa kwa siku nne mfululizo. Taarifa kutoka kundi hilo zaarifu kuwa wamerudi nyuma ili kujipanga vema zaidi. Mji wa Gao ulishuhudia mashambulizi makubwa ya anga jumapili iliopita ambapo mji wa Duenze ulishambuliwa jana. Wanajeshi wa ardhini wameanza kuwasili nchini Mali kukabiliana na wapiganaji hao wa makundi ya Kiislam.

Kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa kilichokuwa Tchad chaelekea nchini Mali
Kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa kilichokuwa Tchad chaelekea nchini Mali REUTERS/ECPAD/Adj. Nicolas Richard/Handout
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wapiganaji wa kundi la Jihad wameendesha mashambulizi makali jana na kuuteka mji wa Diabali uliopo katika katika mwa Mali baada ya makabiliano na jeshi la Mali, operesheni inayo tajwa kuongozwa na Abou Zeid mmoja kati ya viongozi wa kundi Alqaeda Maghreb

Kulingana na waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Ledrian operesheni za anga katika mji wa Timbuktu bado hazijaanzishwa, lakini kwa sasa kila kitu kinakwenda kama ilivyopangwa.

Wakati huo huo serikali ya Algeria kupitia waziri wake wa mambo ya nje imetangaza kuufunga mpaka wake na Mali baada ya ziara ya waziri mkuu wa Mali nchini humo Django Cissoko, huku Mauritania ikitangaza kuwa haitoignia katika mzozo huo, kama anavyoeleza hapa naibu mwenyekiti wa chama tawala cha UPR, Mohamed Aldorma

Nchi kadhaa zimekubali kushiriki katika operesheni ya kikosi cha ECOWAS huko Mali, Guinea imetsngaza ujio wa kikosi cha wanajeshi 125, Ghana ikiwatuma wanajeshi wataalamu wa maswala ya ujenzi wapatao 120, huku wanajeshi 600 wa Nigeria wakitarajiwa kuwasili nchini Mali kabla ya Juma hili kumalizika..

Ufaransa imetangaza kuitisha kikao cha dharula cha mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Juma hili kuzungumzia mzozo wa Mali. Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Ledrian anataraji kuongoza shughuli za mazishi ya Luteni Damien Boiteux mwanajeshi wa Ufaransa alieuawa siku ya Ijumaa iliopita.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.