Pata taarifa kuu
MAREKANI

Wabunge wapitisha sheria huku Rais Obama akiwahakikishia wananchi watatekeleza yote yaliyoafikiwa

Kizungumkuti juu ya kupita au la kwa sheria ya kuzui kupanda kwa kodi na mpango wa kubana matumizi ya fedha nchini Marekani kimepata ufumbuzi baada ya wabunge wengi kupiga kura ya kupitisha sheria hizo na kumaliza hali hiyo ya sintofahamu. Wabunge nchini Marekani wamekuwa kwenye mvutano mkali punde tu baada ya kumalizika kwa sherehe za Noeli na kuwalazimu kurejea haraka kuendelea na mchakato wa kupitishwa kwa sheria hizo ili kunusuru bajeti ya serikali.

Rais wa Marekani Barack Obama akiwa na Makamu wa Rais Joe Biden punde baada ya Baraza la Seneti kupitisha sheria zilizonusuru bajeti ya nchi hiyo
Rais wa Marekani Barack Obama akiwa na Makamu wa Rais Joe Biden punde baada ya Baraza la Seneti kupitisha sheria zilizonusuru bajeti ya nchi hiyo REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Wasiwasi mkubwa ulikuwa umetanda kutokana na pande mbili zenye wabunge wengi Republican na Democrats kutunishiana misuli kutokana na kila upande kushikilia msimamo wake hatua ambayo imeliingiza taifa hilo kwenye hofu ya kutetereka kiuchumi.

Makamu wa Rais Joe Biden ndiye ambaye ameshiriki kwa kiasi kikubwa kuhakikisha ananusuru upitishwaji wa sheria hizo baada ya kukutana na Wabunge wa Republican ambao walikubali kuweka tofauti zao na Democrats kando na kuangalia maslahi ya Umma.

Congress imepitisha sheria hizo baada ya hapo awali Bunge la Seneti kuridhia hatua kama hiyo kwa kupiga kura za ndiyo 257 dhidi ya kura za hapana 167 na hivyo kuonesha mwelekeo mwema.

Licha ya kupitishwa kwa sheria hizo lakini kumekuwa na mfarakano wa kisiasa huku wabunge wa Chama Cha Republican wakitaka marekebisho kadhaa yafanyike ili sheria hizo ziwe na manufaa kwa wananchi.

Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kufurahishwa na hatua ambayo imefanywa na wabunge wa nchi hizi na kuahidi atasaini sheria hiyo ambayo itaongeza kiwango cha ulipaji kodi kwa asilimia mbili kwa matajiri.

Obama anasema sheria hiyo itasaidia wananchi wenye uwezo wa kati na mdogo kuweza kuishi vizuri kutokana na kutobanwa sana na mzigo mkubwa wa kodi kama ambavyo ilivyo kwa sasa hali inayowafanya wazidi kuwa tegemezi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.