Pata taarifa kuu
DRC-MAREKANI

Kundi la M23 lakanusha madai ya kutekeleza uhalifu dhidi ya binadamu kwenye maeneo wanayoyashikilia

Kundi la Waasi la M23 ambalo linapambana na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC limeshangazwa na hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC kuwawekeza vikwazo, kuzuia mali zao na kuwazuia kusafiri baadhi ya Viongozi wao.

Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 ambalo Viongozi wake wamewekewa vikwazo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC
Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 ambalo Viongozi wake wamewekewa vikwazo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Kundi la M23 limesema ushahidi ambao umetumika kuwawekea vikwazo haukuwa sahihi na badala yake wangeomba Baraza la Usalama lingetuma ujumbe kwenda kwenye maeneo ambayo wanayashikilia na kujionea ukweli halisi uliopo huko.

Msemaji wa Kisiasa wa Kundi la M23 Bertrand Bisimwa ndiye ambaye amekiri kushangazwa kwa Kundi hilo na hatua ya kuwekea vikwazo viongozi wao ambao ni Jean-Marie Runiga Lugerero na Luteni kanali Eric Badege.

Bisimwa amesema wao hawajawahi kukiuka Haki za Binadamu kama ambavyo wamekuwa wakituhumiwa na badala yake wamekuwa mstari wa mbele kuwalinda wananchi na kushirikiana nao kila sehemu ambayo wanachukua utawala wa eneo husika.

Msemaji wa Kisiasa wa M23 amebainisha wanawasiwasi na ushahidi ambao umetumiwa na Baraza la Usalama la kuwatuhumu wao kuendelea kutenda visa vya uhalifu wa kivita kwa wananchi pamoja na kutekeleza ubakaji.

Bisimwa ametoa wito kwa Baraza la Usalama kuwahusishwa kwenye mchakato wao wa kusaka ushahidi ili kujua ukweli wa kile ambacho kinaendelea kwenye maeneo ambayo wamekuwa wakiyashikilia hasa Mashariki mwa DRC.

Bisimwa hakuishia hapo lakini amesema wapo wapo tayari hata kufikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC iwapo watabainika wametenda makosa ya uhalifu wa kivita kama ambavyo wanatuhumiwa.

Utetezi wa Kundi la Waasi la M23 umekuja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC kutangaza vikwazo kwa viongozi wake na kuchukua mali zao na pamoja na kundi rafiki kwao la nchini Rwanda FDLR.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.