Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Waasi wa Seleka wataka Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize aondoke madarakani

Kundi la Waasi la Seleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati limeendelea kutoa wito wa kutaka Rais Francois Bozize aondoke madarakani huku wakiendelea kukaribia Jiji la Bangui bila ya kukosa Upinzani wa aina yoyote.

Waasi wa Kundi la Seleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakisonga mbele kuelekea Mji Mkuu Bangui
Waasi wa Kundi la Seleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakisonga mbele kuelekea Mji Mkuu Bangui
Matangazo ya kibiashara

Waasi wa Seleka wamesalia kilometa mia moja sitini kufika Jiji la Bangui ikiwa ni majuma matatu tangu wameanza harakati zao za kuteka Miji kadhaa katika nchi hiyo wakishinikiza kuondoka madarakani kwa serikali ya Rais Bozize.

Msemaji wa Kundi la Seleka Eric Massi amesema wao wanachokihitaji kwa sasa ni kuondoka madarakani kwa Rais Bozize na hawana mpango tena wa kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa kama ambavyo Kiongozi huyo amependekeza.

Kundi la Seleka limesema hakutakuwa na mazungumzo yoyote na serikali kwa sasa kutokana na hapo awali serikali ya Bangui kukataa kuketi mezani nao wakipuuza madai waliyokuwa nayo.

Kufuatia Kundi la Waasi la Seleka kuendelea kusonga mbele ya kuanza kupiga hodi kukaribia Bangui hofu kubwa imetanda katika Jiji hilo huku wananchi wengi wakiendelea kujifungia kwenye majumba yao.

Serikali ilitangaza hali ya hatari na kuwataka wananchi kuacha kutembea usiku wakihofia Waasi wa Seleka huenda wakavamia wakato wowote kitu ambacho kitahatarisha usalama wa raia watakaokuwa wanazagaa.

Taarifa zinaeleza wanajeshi mia moja ishirini kutoka Congo Brazzaville wameingia Bangui kuwasaidia wanajeshi wa serikali kuimarisha ulinzi na kujiweka tayari kwa mapigano ambayo yanaweza kuzuka pindi Waasi wa Seleka watakapokuwa wanataka kuuteka Mji huo.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amezungumza kwa njia ya simu na Rais Bozize na kumtaka kufanya kila linalowezekana ili kufanya mazungumzo na Kundi la Seleka ili kumaliza hali ya sintofahamu iliyozuka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.