Pata taarifa kuu
MISRI

Wapinzani wapinga matokeo ya kura ya maoni nchini Misri

Upinzani nchini Misri umetangaza nia yao ya kukata rufaa kupinga matokeo ya kura ya maoni ambayo yameipitisha rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo katika duru la pili ambalo limefanyika mwishoni mwa juma.

bloomberg.com
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Rais Mohamed Morsi na vyama ambavyo vinamuunga mkono vimefanikiwa kushinda kwenye kura hiyo ya maoni kwa kupata asilimia sitini na nne ya kura ambazo zimepingwa kwenye duru la pili licha ya watu wachache kujitokeza.

Wapinzani wametoa wito wa kuitaka Tume ya uchaguzi kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini udanganyifu uliofanyika na kisha kutoa matokeo sahihi kwa mustakabali wa Taifa hilo.

Aidha Msemaji wa Kundi la Ukombozi la Upinzani maarufu kama National Salvation Front Khaled Dawoud amesema kura hiyo ya maoni siyo mwisho wa harakati zao katika kudai mabadiliko ya kweli ndani ya Misri hata ikiwa serikali yao itaendelea kuwagandamiza.

Mpaka sasa Rais Mursi na Wafuasi wake bado wanashikilia msimamo wao kuwa rasimu hiyo imebeba mambo madhubuti yatakayosaidia kuziba mapengo yaliyopelekea kuangushwa kwa utawala wa Hosni Mubarak kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.