Pata taarifa kuu
SYRIA

Wakristo waandamwa na vitisho toka kwa waasi wa serkali ya Syria

Wakati wakikristo duniani kote wakijiandaa kuadhimisha sikukuu ya krismas, waumini wa dini hiyo wanaoishi katika eneo la Hama nchini Syria wameendelea kupata vitisho toka kwa waasi wa kiislamu wa kiislamu ambao wameapa kuwavamia ikiwa hawataungana nao katika harakati za kuung'oa madarakani utawala wa Rais wa nchi hiyo Bashar Al Assad.

fanaticforjesus.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

Waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria wamesema maeneo yenye idadi kubwa ya wakristo yamekuwa yakikumbwa na mashambulizi na wengi wamekimbia makazi yao licha ya kiongozi wa dhehebu la Orthodox kutoa wito wa waumini hao kusalia katika maeneo yao na kuonesha msimamo wa imani yao.

Wakristo wapatao milioni moja na laki nane wanaishi nchini Syria, na wengi wao wamebaki kati bila kuunga mkono upande wowote katika vita inayoendelea kutokana na kuhofia kuteswa na vikundi vya kiislamu.

Ripoti ya wachunguzi wa tume ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hivi karibuni ilibaini machafuko yanayotokana na mgogoro wa Syria yamekuwa yakihusishwa na udini na kuibua vitisho katika jamii.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.