Pata taarifa kuu
URUSI-EU

Rais wa Urusi akutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya

Rais wa Urusi Vladimir Putin anakutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya EU katika mazungumzo ya leo ijumaa yanayolenga kugusia maswala ya kibiashara, haki za binadamu na machafuko yanayoendelea nchini Syria.

REUTERS/Grigory Dukor
Matangazo ya kibiashara

Rais wa EU Herman Van Rompuy na Mkuu wa Tume ya Ulaya Jose Manuel Barroso wamemkaribisha Rais Putin muda mfupi hii leo kabla ya kuingia katika mkutano huo.

Viongozi wa EU wamekuwa wakipata shinikizo toka kwa wabunge na makundi ya haki za binadamu kutilia mkazo maswala ya haki za binadamu katika mkutano huo licha ya Putin kushutumiwa kuendesha utawala wa kimabavu nchini mwake.

Mapema wiki hii Van Rompuy alisema anatarajia kuwa mazungumzo hayo yatakuwa na mchango mkubwa katika maendeleo na suluhu ya migogoro inayotatiza hivi sasa.

Suala la haki za binadamu linapewa kipaumbele na EU lakini Rais Putin amekuwa akizishutumu nchi za magharibi kwa kuingilia maswala ya ndani na kuunga mkono makundi ya wapinzani nchini Urusi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.