Pata taarifa kuu
SUDAN-UN-AU

Mohamed Ibn Chambas kuongoza mpango wa amani wa UN na AU nchini Sudan

Umoja wa Afrika AU na Umoja wa Mataifa UN umemteua kiongozi wa zamani wa Afrika Magharibi Mohamed Ibn Chambas kuongoza mpango wa dunia wa amani katika jimbo la Dahfur nchini Sudan ili kutafuta ya mzozo katika eneo hilo ambalo limegubikwa na machafuko kwa takribani miaka kumi sasa.

republicoftogo.com
Matangazo ya kibiashara

Uteuzi huo umeelezwa jana alhamisi katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-moon na Mwenyekiti wa AU Nkosazana Dlamini Zuma.

Mohamed Ibn Chambas toka nchini Ghana anarithi mikoba ya Ibrahim Gambari wa Nigeria ambaye amekamilisha muda wake wa kuhudumu katika nafasi hiyo na Chambas anatarajiwa kuongoza wanajeshi elfu ishirini na moja na Maofisa wa polisi katika mpango wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Dahfur (UNAMID).

Chambas amewahi kuwa mkuu wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afriks Magharibi ECOWAS toka mwaka 2006 mpaka 2009, na pia amewahi kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa ECOWAS.

Wanadiplomasia wa Kiafrika wanaona kuwa uteuzi huo ni sahihi kutokana na uzoefu alionao Chambas hususani juhudi zake za upatanishi nchini Liberia katika vita vya ndani vilivyoikumba nchi hiyo mwaka 1990.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.