Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI

Rais Mteule wa Korea Kusini aahidi kuunda sera madhubuti kulinda usalama wa nchi hiyo

Rais Mteule wa nchini Korea kusini Park Geun-Hye ameahidi kuunda sera madhubuti juu ya usalama wa nchi hiyo wakati huu akitafuta kuwa na mahusiano mazuri na Korea kaskazini. 

Rais mteule wa Korea Kusini Park Geun-Hye
Rais mteule wa Korea Kusini Park Geun-Hye scrippsiij.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwa Mara ya kwanza tangu kunyakua ushindi wa kihistoria nchini humo kwa kuwa rais wa kwanza mwanamke, Park amesema kuwa jaribio la roketi la hivi karibuni lililofanywa na Korea Kaskazini limelenga kutoa vitisho kwa adui zake hali inayodhihirisha kuwa hali ya usalama wa Korea kusini ni tete.

Kufuatia ushindi wa mwanamama huyo wachambuzi wa siasa wanaona kuwa ni hatua mpya katika siasa za Korea Kusini ambapo huenda ikabadili mwelekeo wa siasa za Korea kusini na kuwahusisha zaidi wanawake katika masuala ya uongozi.

Kwa upande mwingine wachambuzi wanaona kuwa mwanamke huyu atakabiliwa na changamoto kubwa ya kufumua mfumo dume wa uongozi uliokuwepo na kuleta mfumo utakaohusisha jinsi zote kwa manufaa ya taifa hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.