Pata taarifa kuu
MALI

Baraza la Usalama la umoja wa mataifa kupiga kura ya kuidhinisha jeshi la Africa Kaskazini mwa Mali

Baraza la usala ma la umoja wa mataifa UN huenda likapiga kura leo Alhamisi kuhusu pendekezo la kupeleka jeshi la pamoja la Afrika nchini Mali kwaajili ya kujiandaa kukabiliana na wanamgambo wenyeuhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabab Kaskazini mwa nchi hiyo. 

allgedo.com
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa ilitarajiwa kupeleka pendekezo lake jipya kuhusu Mali kwa wajumbe wengine 14 wa baraza hilo jana Jumatano baada ya kuwa imeshiriki mazungumzo ya majuma kadhaa na Jamhuri ya Muungano ya Mali.

Wanadiplomasia wa Marekani wameelezea shaka yao kuhusu jeshi hilo la umoja wa Afrika kama litakuwa imara zaidi kupambana na wapiganaji wa tawi la Al Qaeda la AQIM na lile la MUJAO.

Kundi la waasi wa kiislamu wenye msimamo mkali waliteka eneo la Kaskazini mwa Mali katika mapinduzi ya kijeshi yasiyo mwaga damu mnamo mwezi Machi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.