Pata taarifa kuu
Syria-Machafuko

Wakimbizi waendelea kutangatanga wakati mashambulizi yakizidi kupamba moto nchini Syria

Makabiliano makali yameendelea kushuhudiwa katika kambi ya wakimbizi wa Palestina jijini Damascus nchini Syria kati ya wafuasi na wapinzani wa rais wa nchi hiyo Bashar Al Assad. Watu zaidi ya tisini wanahofiwa kuuawa jana jumanne kutokana na makabiliano yanayoendelea kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Serikali vinadaiwa kutekeleza mashambulizi kadhaa ya anga katika mji wa Yarmuk kusini mwa Damascus wakati watu wakiendelea kuyakimbia maeneo hayo.

Shirika linaloshughilikia misaada ndani ya umoja wa mataifa limesema takribani nusu ya wakazi wa Yarmuk zaidi ya laki moja na kumi na mbili elfu wamekimbia kutokana na machafuko hayo.

Shirika la chakula duniani limeonya kuwa machafuko hayo yanafanya hali kuwa ngumu zaidi kwa zoezi la kutoa msaada wa chakula kwa raia linakwamishwa na mapigano hayo.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa wanajeshi wa serikali wanatumia ndege za kivita kushambulia eneo hilo baada ya kuziingira kambi hiyo ya Yarmouk.

Aidha Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Ahmet Davutoglu amemtaka mshirika wa karibu wa Syria, Iran kupeleka ujumbe kwa Rais wa nchi hiyo, Bashar Assad kuacha kushambulia watu wake.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.