Pata taarifa kuu
Misri-Maandamano

Upinzani nchini Misri, watowa wito wa maandamano zaidi siku ya jumanne

Upinzani nchini Misri unatarajiwa kufanya maandamano makubwa hiyo kesho hatua inayokuja baada ya Vyama Vya Kiislam ambavyo vinamuunga mkono Rais Mohamed Morsi kujitangaza kupata ushindi kwenye duru ya kwanza ya kura ya maoni ya kupitisha rasimu ya katiba mpya.

Polisi wakipiga doria kuzuia maandamano ya upinzani
Polisi wakipiga doria kuzuia maandamano ya upinzani REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Upinzani umelaani namna ambavyo kura hiyo iliendeshwa na umejiapiza kuingia mtaani kwa ajili ya kutetea uhuru wao na kupiga vita udanganyifu huku wakishinikiza wananchi waukatae muswada wa katiba.

Vyama vinavyomuunga mkono Rais Morsi vimejigamba kupata ushindi wa asilimia hamisni na saba kura za ndiyo, katika uchafuzi uliopigwa desemba 16 mwaka 2012, jambo ambalo linapingwa vikali na upinzani

Upinzani nchini humo umejitokeza na kupinga matokeo hayo ambayo sio rasmi, na sasa wametowa wito kwa wafuasi kuandamana kesho jumanne nchi nzima, kupinga hatuwa hiyo ya kupiga kura ya maoni ambayo inataraji kufanyika mara nyingine tena siku ya Jumamosi juma hili.

Upinzani uliojumuika katika muungano wa National Front, umesema utashiriki katika uchaguzi huo iwapo madai yao yatatekelezwa.

Upinzani huo unataka uwepo wa ma jaji katika vituo vya kupigia kura, baada ya waangalizi kuona ma jaji wakikosekana katika vituo kadhaa vya kupigia kura.

mbali na hayo upinzani huo umeitaka tume inayo simamia uchaguzi huo kuhakikisha dosari zote zilizo jitokeza katika awamu ya kwanza zinafanyiwa kazi, huku mashtaka yaliotolewa na mashirika kadhaa ya kirai pia yanafanyiwa kazi.

wachambuzi wa maswala ya siasa, wanaona kuwa baadhi ya madai ya upinzani, hayawezi kutekelezwa kwakuwa miongoni mwa

.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.