Pata taarifa kuu
BURUNDI

Mahakama nchini Burundi yaahirisha kesi ya mauaji ya mwanaharakati Ernest Manirumva

Kesi ya mauaji ya mwanaharakati na mtetezi wa kupiga vita rushwa nchini Burundi Ernest Manirumva aliyeuawa mwaka 2009 imeahirishwa hadi Novemba 29 mwaka huu baada ya kusikilizwa jana na mahakama ya jijini Bujumbura, huku wanadiplomasia kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia kwa umakini kesi hiyo. 

Mwanaharakati wa Burundi  Ernest Manirumva
Mwanaharakati wa Burundi Ernest Manirumva article.wn.com
Matangazo ya kibiashara

Makamu mwenyekiti wa shirika linalopiga vita rushwa na ubadhirifu wa mali ya Umma nchini Burundi OLUCOME, Ernest Manirumva aliuawa kwa kuchomwa kisu akiwa nyumbani kwake mwezi April mwaka 2009 na kundi la watu ambao walichukuwa faili kadhaa nyumbani kwa marehemu baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Mwezi Mei mwaka 2012 mahakama kuu nchini burundi iliwahukumu kifungo cha maisha jela watu wanane waliohusishwa na kifo hicho, huku wengine sita wakiwemo polisi watatu wakihukumiwa kifungo cha miaka kati ya 10 na 20 kwa kosa la kushiriki kwenye mauaji na kukosa kumsaidia mtu aliyekuwa hatarini hukumu ambayo ilikemewa vikali na kutupiliwa mbali na wanaharakati watetezi wa haki za binadamu ambao walikata rufaa.

Ikisikilizwa kwa mara ya kwanza jana na mahakama ya rufaa jijini Bujumbura, kesi hiyo ilidumu kwa muda wa saa mbili ambapo wanadiplomasia kutoka mataifa mbalimbali walikuwepo mahakamani kuhudhuria kesi hiyo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.