Pata taarifa kuu
SYRIA

Waasi wa kiislamu mjini Allepo wapinga muungano wa upinzani ulioundwa na mataifa ya magharibi

Kundi la waasi lenye msimamo mkali wa kiislamu mjini Allepo nchini Syria linasema kuwa haliungi mkono muungano wa upinzani ulioundwa wiki iliyopita na Mataifa ya Magharibi kupambana na uongozi wa rais Bashar Al Assad.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Waasi hao wa kiislamu sasa wanasema kuwa lengo lao ni kuunda serikali ya kiislamu nchini Syria, huku Umoja wa Ulaya ukiweka wazi kuwa unaunga mkono muungano huo wa upinzani kama unawakilisha watu wa Syria na mapambano dhidi ya rais Assad.

Katika tangazo la Waasi hao la Novemba 11 wamekataa kuingiliwa na taifa lolote au baraza lolote katika masuala ya ndani ya Syria.

Hatua ya waasi wa kiislamu kutangaza kupingana na muungano wa upinzani wa Syria inatazamwa kama pigo kwa muuungano huo na baadhi ya wachambuzi wa sayansi ya siasa kama Hilal Khashan,wa chuo kikuu cha Marekani cha Beirut.

Kwa sababu hiyo wamarekani na Uingereza waliona busara kabla ya kuutambua muungano kama muwakilishi pekee halali wa watu wa Syria.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.