Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-GAZA

Israeli yaendeleza mashambulizi ya anga Ukanda wa Gaza, Netanyahu aapa kulinda usalama wa raia

Nchi ya Israeli imeendelea na mashambulizi yake ya anga kwa siku ya pili mfululizo kwenye eneo la ukanda wa Gaza na kuendelea kuzusha hofu kuhusu hali ya usalama kwenye eneo hilo pamoja na uhusiano kati yake na Palestina huku viongozi mbalimbali wakiendelea kulaani kile kinachoendelea.

REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yamezidi kufuatia kurushwa kwa makombora zaidi ya sita toka eneo la ukanda wa gaza ambayo israel imesema ni toka kwa wapiganaji wa kundi la Hamas ambalo limekuwa likiendesha ugaidi dhidi ya taifa lao.

Nchi ya Misri imekuwa mstari wa mbele kusuluhisha mgogoro huo na rais wa Israeli Shimon Peres ameeleza mchango wa Misri in mchango mkubwa wa kumaliza machafuko hayo.

Hata hivyo rais wa Misri Mohamed Morsi amelaani kile kinachofanywa na Israeli huku Israeli ikiahidi kusitisha mashambulizi hayo siku ya leo ijumaa wakati rais huyo wa Misri atakuwa akizuru Israeli.

Kwa upande wake waziri mkuu wa Israel benjamin Netanyahu ameendelea kusisitiza nchi yake kufanya mashambulizi zaidi kulinda mipaka yake dhidi ya magaidi.

Licha ya mashambulizi hayo kundi la Hamas lenyewe limesema litaendelea kujibu mashambulizi kwa kila kombora ambalo litarushwa na majeshi ya Israel.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.