Pata taarifa kuu
MALI

Viongozi Afrika waridhia kupeleka askari 3,3000 nchini Mali

Viongozi wa Afrika waliokutana jana mjini Abuja wamekubaliana kupelekwa kwa kikosi cha askari 3,300 nchini Mali, kwa kipindi cha mwaka mmoja kukabiliana na waasi wa kiislamu wanaoshikilia eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Kupelekwa kwa viokosi hivyo kunakuja kufuatia nchi wanachama wa nchi za magharibi mwa afrika, ECOWAS kutangaza kuingilia kati mzozo wa Mali na kuomba ridhaa toka umoja wa Afrika AU na baraza la usalama la Umoja wa mataifa UN ambao waliridhia na mpango huo.

Itakumbukwa kuwa tangu tarehe 24 Septemba mwaka huu, serikali ya Mali iliomba majeshi ya Jumuiya ya Afrika magharibi kuingilia kijeshi mgogoro ulioko nchini mali.

Wakati huohuo Chama cha upinzani nchini Senegal cha PDS kimelalamikia serikali ya nchi hiyo kuendelea kuwakamata viongozi mbalimbali waliokuwa chini ya utawala wa rais Abdoulaye Wade kwa tuhuma za rushwa.

Kamati maalu ya polisi wa bunge nchini humo imeanzisha uchunguzi rasmi dhidi ya waliokuwa mawaziri wakati wa utawala wa Wade ambao wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kujilimbikizia mali wakati wakiwa viongozi.

Miongozi mwa walioitwa mbele ya kamati hiyo ni pamoja na mtoto wa rais Wade, Karim Wade ambaye ametakiwa kutokea mbele ya kamati hiyo siku ya alhamisi kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.