Pata taarifa kuu
Syria-Israeli

Israeli yashambulia Syria, Ban Ki Moon aonya

Nchi ya Israeli imefanya mashambulizi ya roketi kwenye ardhi ya Syria kama onyo kwa nchi hiyo kufuatia mwishoni mwa juma eneo lenye mgogoro la Golan kushambuliwa kwa roketi toka upande wa Syria.

Image: Russia Today
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa majeshi ya Israel Avil Leibivich amethibitisha nchi yake kufanya mashambulizi kama onyo kwenye ardhi ya Syria na kuonya kuwa iwapo nchi hiyo itaendelea kushambulia maeneo yake italazimika kuingia kwenye vita na Syria.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon ameonya kuhusu mashambulizi hayo na kwamba huenda yakasabisha nchi hizo mbili kuingia vitani na kusababisha mgogoro huwa kuwa mkubwa zaidi.

Katika hatua nyingine viongozi wa upinzani nchini Syria waliokuwa wanakutana mjini Doha nchini Qatar kwa kauli moja wamekubaliana kuyajumuisha makundi mengine yanayopigana nchini humo na kuteua rais mpya wa baraza la mapinduzi nchini humo SNC.

Makubaliano hayo yamekuja kufuatia shinikizo toka kwa mataifa ya magahribi yakihoji uhalali wa baraza la awali la SNC kwakuwa lilikuwa halijumuishi makundi mengine ya wapiganaji jambo ambalo lilifanya wakose misaada toka kwa nchi za magahribi.

Mara baada ya uteuzi wake rais mpya wa SNC George Sabra amesema kuwa sasa haina haja kwa nchi zinazowaunga mkono kuwasaidia kwa vifaa vya kijeshi kuipindua serikali ya rais Bashar al-Asad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.